• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Msikimbilie Kuuza Ufuta kwa Chomachoma

Posted on: May 25th, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya wakulima wa ufuta wasikimbilie kuuza zao hilo kwa wanunuzi wasio rasmi maarufu kwa jina la chomachoma bali wasubiri minada itangazwe mwezi ujao.


“Ninawasihi msikubali kuuza kwa akina chomachoma bali tumieni Mfumo wa Stakabadhi za Mazao Ghalani, tumeona mfumo huu ulivyosaidia kwenye korosho,” amesema.


Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua uwanja mpya wa michezo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.


"Kuna wawakilishi wa Kampuni ya Hyseas International Investment (T) Limited ya kutoka China ambao wamekuja hapa kuonana na uongozi wa Halmashauri. Wamesema watanunua ufuta wote uliolimwa Ruangwa na Nachingwea, ndiyo maana ninawasihi msubiri, msikimbiile kuuza ufuta kwa sasa,” alisisitiza.


Alisema kampuni hiyo imeahidi kuweka vituo vya ununuzi kwenye kata za Mandawa, Nanjaru, Nangurugai, Machang’anja hadi Mbangala ili wakulima wasihangaike kusafirisha ufuta wao. “Tunataka mwaka huu, wakulima wa ufuta nao wapate hela nzuri,” alisema.


Wakati huohuo, Waziri Mkuu amekabidhi mikopo kwa wajasiriamali 42 wanaofanya kazi zao Wilayani Ruangwa ambapo kati yao akinamama lishe ni 39 na akinababa lishe ni watatu.


Mkurugenzi wa kampuni ya Ruangwa Distributors ambayo imetoa mikopo hiyo, Bw. Abdallah Mang’onyola alisema wajasiriamali 30 kati ya 42, wamepokea mikopo ya sh. 200,000 na 12 waliobakia wamepokea mikopo ya sh. 250,000.


Alisema wajasiriamali hao wanatoka kwenye kata saba za Matambalale, Narung’ombe, Mbekenyera, Chibula, Namichiga, Mandawa na Nambilanje.


Akizungumza na wajasiamali hao pamoja na wananchi waliofika kwenye hafla hiyo fupi, Waziri Mkuu alimshukuru Mkurugenzi wa Ruangwa Distributors kwa kutoa mikopo hiyo yenye masharti nafuu na isiyo na riba.


Waziri Mkuu alisema hii ni mara ya pili kwa wajasiriamali wa Wilaya hiyo kupatiwa mikopo. Alitumia fursa hiyo kumshukuru Bw. Mpaluka Hashim Mtopela wa kampuni ya Sasalema ambaye awali alitoa mikopo ya sh. milioni 25 kwa wajasiriamali 89.

(mwisho)




Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa