Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma azindua Chanjo ya kuwakinga wanawake dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi( HPV) leo April 22, 2024 katika shule ya msingi Likangara na kutoa wito kwa jamii kuamini chanjo hizo ili kuwa na jamii yenye Afya bora kwani kinga ni bora kuliko tiba.
" Unaposhughulika na afya za watu kinga ni bora kuliko tiba, hata kwa Mataifa ya wenzetu wanapambana na magonjwa kwa kinga na sio tiba hivyo tuige mfano wao" Amesema Ngoma.
Saratani ya mlango wa kizazi ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika na huongoza kwa kusabisha vifo vingi vya wanawake hivyo basi Idara ya Afya Wilaya ya Ruangwa imepanga kutoa chanjo kwa watoto 11,561 waliopo shuleni na watoto 3,000 waliopo mtaani wenye umri kuanzia miaka 9 hadi 14.
Chanjo hii imeanza kutolewa leo Aprili 22, 2024 katika maeneo tofauti tofauti barani Afrika na itaishia Aprili 28, 2024 na mkakati wa serikali ni kufikisha 80% ya watoto ambao watapatiwa chanjo hiyo kwa nchi nzima.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa