Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma awataka viongozi katika ngazi ya vijiji kusimamia na kutekeleza mpango wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi ili kuweza kuleta tija tarajiwa.
" Suala la kupima ni jambo moja na suala la kusimamia ni suala jingine, najua changamoto zipo hasa mwingiliano wa maeneo katika vijiji, utakuta eneo ambalo limetengwa kwa lengo la kujenga Zahanati ya kijiji, pamejengwa soko au ghala kwahiyo Serikali ya kijiji ni jukumu lenu sasa kusimamia mipango yote ili kuleta tija katika kijiji husika" Amesema Ngoma
Ameyasema hayo leo Machi 22, 2024 katika Kikao cha wadau kujadili utekelezaji wa mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi(LTIP) kilichofanyika katika ukumbi wa Ruangwa Pride Hotel wilayani Ruangwa.
Aidha Ngoma ameongeza kwa kusema kuwa upimaji wa ardhi katika vijiji unaambatana na kutunga sheria ndogondogo katika vijiji hivyo ili kuwa mwarobaini wa changamoto zote za usalama wa milki za ardhi vijijini na migogoro ya ardhi hususani kwa wakulima na wafugaji.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa