Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, ameshiriki kupiga kura leo 29 Oktoba 2025 katika Kituo cha RUTESCO, Jimbo la Ruangwa, akitimiza haki yake ya kikatiba katika uchaguzi wa Rais, Mbunge na Madiwani.
Mhe. Ngoma amefika kituoni mapema asubuhi, akiwa sambamba na wananchi wengine waliokuwa wakijitokeza kwa wingi kupiga kura kwa amani na utulivu. Tendo hilo limeonyesha mfano wa uwajibikaji na uzalendo katika kushiriki mchakato wa kidemokrasia unaoendelea nchini kote.
Baada ya kupiga kura, Mhe. Ngoma amewahimiza wananchi wa Ruangwa kujitokeza kwa wingi kutekeleza haki yao ya kikatiba kwa utulivu na upendo. “Nawahimiza wananchi wote wa Ruangwa mjitokeze kwa wingi kupiga kura. Huu ni wakati wa kutumia haki yenu kikatiba kwa amani na utulivu. Tuchague viongozi tunaowaamini bila vurugu, maana uchaguzi ni sehemu ya kuamua mustakabali wa maendeleo ya taifa letu,” amesema.
Aidha, amewataka wananchi kudumisha hali ya amani na mshikamano katika kipindi chote cha uchaguzi, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo na kila mwananchi ana jukumu la kuilinda.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa