Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma apokea Mwenge wa Uhuru leo Mei 28, 2024 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ambao utapitia na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Ruangwa yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.1 za Kitanzania.
Miradi hiyo ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Nangumbu, Mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Michenga, Mradi wa uhifadhi wa mazingira Chimbila "A" Mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji Nandagala, Mradi wa Lishe Nkowe, Mradi wa Kikundi cha Ujenzi cha Vijana( UKAJE) Kilimahewa na Mradi wa barabara ya Dodoma na Majaliwa Complex.
Kwa mwaka 2024 Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ruangwa utakimbizwa zaidi ya kilomita 116.1 katika Kata 11 zenye Vijiji 25.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa