Kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano kimefana kwa uwepo wa matukio mbalimbali ambayo yametumbuizwa na wanafunzi, walimu, wananchi na wazee katika viwanja vya Wandorwa wilayani Ruangwa huku mgeni rasmi akiwa ni Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Maadhimisho hayo yametamatishwa leo Aprili 26, 2024 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushikamana, kuilinda amani ya nchi kwa maendeleo endelevu.
Aidha Mhe. Ngoma ametambua na kupongeza mafanikio makubwa katika sekta ya elimu, Afya, michezo na miundombinu yaliyofanyika ndani ya miaka 3 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya Wilaya ya Ruangwa na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Wazee waliohudhuria sherehe hizo pia hawakusita kutoa ushuhuda wa umuhimu wa Muungano katika kudumisha amani na umoja wa Taifa akiwemo Mzee Juma Omary Namchapwile amesisitiza kwamba Muungano si kitu cha kufanyia mchezo, bali ni kiini cha amani ya Taifa.
“Leo hii tunaonekana tuna amani duniani ni kwa sababu tunaulinda vizuri Muungano huu hivyo asitokee mtu wa kutaka kuutenganisha ule udongo wa Tanganyika na Zanzibar uliochanganywa na hayati Mwl. Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume ulikuwa na maana kubwa ya mtu atakayetaka kuuvunja Muungano huu basi aanze kwanza kuutafuta ule udogo na autenganishe" Amesema Mzee Namchapwile
Ni muhimu kukumbuka kwamba sherehe hizi hufanyika tarehe 26 mwezi wa 4 kila mwaka, huku zikikumbusha uzito na umuhimu wa Muungano ulioanzishwa na waasisi wa Mataifa haya mawili, hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na hayati Sheikh Abeid Aman Karume, kwa kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar na hatimaye kuunda jina Tanzania.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa