Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, ameongoza Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa robo ya pili (Oktoba-Disemba 2024/2025), leo Februari 5, 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kikao hicho kimejadili maendeleo ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe, changamoto zilizopo, na mikakati ya kuboresha huduma za lishe kwa wananchi wa Ruangwa.
Kikao hicho kimejadili, mafanikio na changamoto zilizojitokeza, pamoja na kuweka mbinu bora za kuboresha huduma za lishe wilayani Ruangwa, kikilenga kuhakikisha Wananchi wanapata lishe bora, kupunguza matatizo ya utapiamlo, na kuimarisha afya ya jamii kupitia ushirikiano wa sekta mbalimbali.
Hata hivyo, Mhe. Ngoma amempongeza Afisa Lishe wa Wilaya ya Ruangwa, Ndugu Barikieli Gulamay Duwe, kwa jitihada zake katika kuhakikisha wananchi wanazingatia lishe bora ili kujiepusha na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa virutubishi muhimu.
Aidha, ametoa wito kwa wahudumu wa afya katika hospitali na vituo vya afya wilayani Ruangwa kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa bora muda wote ili kuendelea kuokoa maisha ya wananchi.
Washiriki wa kikao hicho wameeleza dhamira ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha huduma za lishe na afya wilayani humo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa