Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hassan Ngoma amezindua rasmi zoezi la chanjo ya Surua Rubela leo 15 Februari Wilayani Ruangwa.
Ngoma amewaomba wananchi wa Wilaya ya Ruangwa kutumia nguvu ileile waliotumia wazee wetu kuitokomeza surua kwani ni ugonjwa huo ni hatari unaosababisha ulemavu hivyo wananchi wameombwa kuto ruhusu ugonjwa huo kurejea kwenye familia zetu.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya amesema wao kama Halmashauri wamejipanga na taratibu zote zimekamilika na dhamira yao ni kuchanja kwa asilimia mia moja ikibidi zaidi nakumuahidi Mkuu wa Wilaya watafika kote ikiwemo mipakani mwa Wilaya kwani chanjo hii hailengi wanaokaa mijini pekee.
Kwaupande mwingine Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Dr. Feisal Said akizingumzia chanjo hiyo ya Surua Rubela amesema chanjo hiyo walengwa ni watoto chini ya miaka mitano lengo nikuwatengenezea kinga dhidi ya ugonjwa wa surua na rubela, huku lengo nikuchanja zaidi ya watoto 17,242, lakini pia huduma hizo zitatolewa sehemu muhimu kama vile shuleni, kwenye mikusanyiko pia kuna chanjo mkoba na chanjo tembezi, hivyo Mganga Mkuu Dr. Feisal Said ametoa wito Kwa wananchi wajitokeze kwa wingi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa