Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack azindua mpango mkakati wa elimu wa mwaka 2024 na mkakati huo ambao umepokelewa na Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Lindi, tayari kwa utekelezaji
Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 2, 2024 katika hafla ya ugawaji wa Tuzo za Walimu waliofaulisha na Wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao kwa mwaka wa masomo 2023 iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Likangara wilayani Ruangwa.
Hatua hii ni kufauatiwa na upokeaji wa fedha Bilioni 64 kutoka kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.
Aidha, Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa Waratibu wa elimu kuwapa stara, heshima na kuwahudumia walimu ili wafanye kazi zao vyema na wakiwa kwenye mazingira salama sanjari na hayo atoa rai kwa wazazi kusimamia watoto wao ili kupunguza utoro shuleni.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa