Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe Godfrey Zambi amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuwasaidia wajasilimia mali wadogo wadogo ili kuendeleza ujuzi waliokuwa nao wa utenmgenezaji wa bidhaa, hali itakayopelekea kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi.
Pia aliwataka kuhakikisha wanasimamia bidhaa zinazotengenezwa na wajasilimia mali zinakuwa zimekaguliwa na mamlaka ya chakula na dawa kabla azijaingizwa sokoni, alisema bidhaa nyingi zimekosa vitu muhimu kama kuonesha imetengenezwa lini na mwisho wa matumizi yake ni lini.
"Ni muhimu sana kuwasaidia bidhaa zao ziweze kutambulika maana watu wengi sikuhizi awanunui bidhaa mpaka aikague mwisho wa matumizi ya hiyo bidhaa, ;pia watu wanaangalia vitu vilivyotengenezewa hiyo bidhaa wakurugenzi liangalieni hili jambo muwasaidie hawa wajasilimiamali wenu" alisema Mhe,Zambi.
Aliyasema haya alipotembea katika banda la Ruangwa kwenye maeonesho ya nane nane Ngongo, Lindi, maadhimisho haya yanafanyika kitaifa Katika Mkoa wa Lindi ikiwa ni mwaka wake wa mwisho.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa