Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya leo Jumamosi 9, Machi amefanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya Idara ya Elimu Sekondari wilayani Ruangwa.
Ufuatiliaji huo umelenga miradi yote inayoendelea na pia kukagua maeneo ya kuanzisha miradi mipya katika Shule za Sekondari wilayani Ruangwa
Aidha, Mkurugenzi Chonya amesema ameshaomba fedha Serikali kuu ili kuwezesha kumalizia miradi viporo na kuanzisha mingine mipya ili kuhakikisha Sekta ya Elimu Wilaya ya Ruangwa iwe yenye maendeleo makubwa na kuwafanya wanafunzi wasome bila changamoto
Kwa upande mwingine Mkurugenzi Chonya ameweza kufanya ukaguzi wa ujenzi wa taa nne katika kijiji cha Mandawa na kujiridhisha kuwa ujenzi wake unaendelea vizuri.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa