Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya aongoza zoezi la ugawaji mipira 160 leo Machi 5, 2024 katika shule 4 za msingi ambazo ni Kitandi, Dodoma, Likwachu na Chikundi ambapo ametoa rai kwa walimu wa shule hizo kuitumia vizuri na kuitunza mipira hiyo na kuhakikisha michezo inapewa kipaumbele shuleni kwa kuunda timu za shule pasi upendeleo kwa wanafunzi hao ili kuwepo timu bora za shule.
Aidha Chonya ametoa shukrani zake za dhati kwa FIFA, TFF, serikali ya awamu ya sita iliyo chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan bila kumsahau Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kuboresha sekta ya michezo kwa kuwapa kipaumbele wanafunzi kwani michezo nayo ni Afya.
Kwa upande wao walimu wameishukuru serikali kwa kutambua na kuonesha umuhimu wa michezo kwa wanafunzi na kuahidi kuendeleza michezo shuleni ili kuwaimarisha wanafunzi kiafya na kiakili na kuwatengeneze nafasi za ajira kupitia michezo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa