Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya amefanya Kikao cha uwasilishaji wa mada ya biashara ya hewa ukaa na Wenyeviti wa vijiji wa Wilaya ya Ruangwa leo April 8, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Aidha Ndugu Chonya amewataka vijana wazawa wa Ruangwa, biashara ya hewa ukaa kuichukulia kama fursa ya kupata ajira kwani watafundishwa jinsi ya kulinda na kutunza misitu ili kuweza kuiendesha biashara hiyo.
Kabla ya kikao hicho Wenyeviti hao wamepatiwa mafunzo na Afisa misitu wa Wilaya Ndugu Solomon Massangya kuhusu namna ya kutunza, kulinda na kuhifadhi misitu ili kufanikisha biashara ya hewa ukaa.
Pia Chonya amewataka Wenyeviti wa vijiji kuwa tayari na kutoa ushirikiano ili kufanikisha ufanyaji wa biashara ya hewa ukaa katika Wilaya ya Ruangwa.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Andrew Chikongwe ametoa wito kwa Wenyeviti wa vijiji kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kuwaelimisha na kuwaelewesha juu ya biashara ya hewa ukaa na manufaa yake.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa