Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya ameongoza harambee ya kumpongeza Mwanafunzi wa shule ya Msingi Mbekenyera Answabu Abdallah Maloi (13) ambaye ameshiriki mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa na kuwa mmoja wapo katika timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17.
Harambee hiyo imefanyika leo Juni 8, 2024 katika Kikao cha CMT kilichofanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na kupatikana zaidi ya shilingi 270,000/-
Kwa upande wake, Mwanafunzi Answabu Maloi amewashukuru wote waliojitoa kwa ajili yake na kuahidi atafanya vizuri zaidi kwenye masomo na michezo ili kuongeza hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri zaidi katika sekta ya Elimu na Michezo.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa