Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya amefanya Kikao na Kamati ya kuhakiki madeni ya Halmashauri leo Julai 8, 2024 katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkurugenzi.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti Hosea Shibanda ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya madeni kwa jamii, kupata idadi kamili ya wadai ili kuwaweka katika bajeti ya mwaka huu wa fedha na kuweka utaratibu maalum wa kuwalipa wadai hao, pia kuhakiki na kufahamu madeni yenye uhalisia ya wadai ili mwaka huu wa fedha wadai wawekwe kwenye bajeti.
Kamati ilianza ziara yake Machi 11, 2024 katika Kata zote 22 zilizopo wilayani Ruangwa na kuhakiki madeni kwa watumishi wa Serikali, Wazabuni, Wakandarasi, na wananchi wote na kupata jumla kuu ya madeni ya wadai ni shilingi 1,759,909,726.
Katika hatua nyingine, Ndugu Chonya ametoa maagizo kwa Kamati ya kuhakiki madeni ili kuiboresha zaidi, Kamati ipitie vizuri madeni ya Watumishi na kukaa na Afisa utumishi, Kamati ikutane na Mhandisi ili kupitia madeni ya Wazabuni hadi kwa wale ambao bado hawajajiorodhesha, Kamati iorodheshe watu wanaodaiwa na Halmashauri kama vile watu wa kodi mbalimbali, Kamati ikae na muweka hazina, Mkaguzi wa ndani na Mhasibu ili kujua ni madeni gani ambayo tayari yameshalipwa, pia Kamati ikae na Wakuu wa idara zote ili kujua Watumishi wanaoidai Halmashauri.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wilaya ya Ruangwa Ndugu Thabit Wailala ameishukuru Kamati kwa ushirikiano mkubwa na kufanya kazi kwa ufanisi na weredi mkubwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa