Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Ndugu Maisha Mtipa, ameitembelea timu ya Ruangwa leo 17 Agosti 2025 katika mashindano ya SHIMISEMITA jijini Tanga.
Akizungumza na wachezaji katika viwanja vya Tanga Tech, Mtipa amesema amefurahishwa na namna timu hiyo ilivyojipanga kushiriki mashindano na akasisitiza dhamira yake ya kushirikiana nao katika kila hatua.
Aidha, kama kielelezo cha mshikamano wake, Mtipa amekabidhi kiasi cha shilingi 200,000/= kwa ajili ya kugharamia mahitaji mbalimbali ya timu wakati wa mashindano hayo. Ametumia nafasi hiyo kuwatia moyo wachezaji, akiwataka kudumisha nidhamu, mshikamano na ari ya ushindani ili kuibua heshima kwa Halmashauri ya Ruangwa.
Sambamba na hilo, Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Ruangwa, Ndugu Shadhiri Msungu, ametoa shukrani kwa niaba ya timu, akisema msaada huo umewatia nguvu na kuongeza morali ya kushindana.
Hata hivyo, wachezaji wa Ruangwa wameonesha shauku na ari ya kupambana, wakiahidi kupigania ushindi huku wakipokea hamasa kutoka kwa viongozi wao na wadau wa michezo.
Ikumbukwe, Mashindano ya SHIMISEMITA 2025 yanaendelea jijini Tanga yakihusisha timu kutoka Halmashauri mbalimbali nchini yakiwa na lengo la kukuza mshikamano na kuimarisha michezo miongoni mwa watumishi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa