Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya amekabidhiwa vifaa vya TEHAMA na Kampuni ya Reneal International Education Outreach chini ya Mkurugenzi Ndugu David Nyangaka zitakazotumika katika shule za Sekondari wilayani Ruangwa.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo Julai 6, 2024 na Juma Mshihiri ambaye ni fundi wa vifaa vya TEHAMA kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.
Aidha, vifaa hivyo ni pamoja na Komputa mpakato (Laptop) 100, Vihifadhia nukuu na vifaa vya kujifunzia (Server) 5, vifaa vya kutunza umeme (UPS) 5, na vifaa vya kudhibiti umeme (Regulator) 5.
Shule zilizokabidhiwa vifaa vya TEHAMA ni tano zenye kidato cha tano na sita kwa Wilaya ya Ruangwa, ambazo ni shule ya Sekondari Hawa Mchopa, Lucas Malia, Nkowe, Ruangwa na Mbekenyera.
Katika hatua nyingine, Ndugu Frank Fabian Chonya amewataka Wakuu wa shule hizo kujenga vizuri vyumba maalumu kwa ajili ya matumizi ya komputa mpakato hizo ili wanafunzi waweze kuvutiwa kuingia kujisomea.
Aidha, Ndugu Chonya amesisitiza kwa kusema kuwa komputa mpakato hizo zitumike vizuri na zitunzwe ipasavyo ili ziweze kupandisha ufaulu wa wanafunzi katika Wilaya ya Ruangwa.
"Kwa msaada wa hizi Laptop, Ruangwa sasa tunaenda kuwa namba moja kitaifa kwa ufaulu wa Kidato cha sita" amesema Chonya.
Naye, Mkuu wa shule ya Sekondari Lucas Malia Gladness Makongwa kwa niaba ya Wakuu wa shule za Sekondari zilizonufaika na vifaa hivyo vya TEHAMA ameishukuru Kampuni ya Reneal International Education Outreach kwa msaada huo na kumuahidi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuyatekeleza yale yote aliyoyaagiza kwao ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa