Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Goodluck Mlinga, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack. Maadhimisho haya yamefanyika leo, tarehe 1 Mei 2025, katika Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mlinga ameipongeza jamii ya wafanyakazi kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Mkoa wa Lindi na taifa kwa ujumla, amehimiza ushirikiano kati ya waajiri na wafanyakazi, akisisitiza kuwa mahusiano bora kazini ni msingi wa ufanisi na tija katika taasisi na mashirika.
Aidha, amewataka waajiri kuhakikisha mazingira salama na yenye staha kwa wafanyakazi, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda na kuheshimu haki za msingi za wafanyakazi kama sehemu ya ujenzi wa jamii yenye usawa na mshikamano.
Nitumie nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi wote kwa kazi kubwa mnayoifanya kila siku katika kujenga taifa letu, ushirikiano kati ya waajiri na wafanyakazi ni msingi wa mafanikio ya kiuchumi na kijamii, Serikali itaendelea kusimamia haki za wafanyakazi na kuhakikisha mazingira bora ya kazi kwa wote.”amesema Mhe. Mlinga.
Shughuli hiyo imejumuisha maandamano ya amani, nyimbo za kuhamasisha mshikamano, pamoja na burudani mbalimbali zikilenga kukuza ari ya kufanya kazi kwa bidii, washiriki wameonesha mshikamano wa hali ya juu na utayari wa kuendelea kushiriki katika maendeleo ya Taifa.
Ikumbukwe, sherehe hizi huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Mei Duniani kote kwa lengo la kutambua mchango wa wafanyakazi katika ustawi wa jamii. Zilianza rasmi mwaka 1889 kufuatia azimio la Kongamano la Kimataifa la Kazi, na zimeendelea kuwa ishara ya mshikamano na mapambano ya kupigania haki za wafanyakazi.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Masilahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki.”
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa