Mkoa wa Lindi Leo Jumatano umeungana na mikoa mingine na Taifa kwa ujumla kufanya sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Familia Kimataifa ambayo huadhimishwa tarehe 15 Mei ya kila mwaka.
Siku ya Maadhimisho ya kimataifa ya familia terehe 15 Mei Kimkoa inafanyika Wilaya ya Mtama katika viwanja vya soko la majengo
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu "Tukubali tofauti zetu kwenye familia kuimarisha malezi ya watoto" yamefanyika katika viwanja vya Soko la Majengo, Halmashauri ya Mtama na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi, wanafunzi na wananchi.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga.
Aidha Mhe. Ndemanga ametoa wito kwa wazazi kudumisha upendo katika familia, uvumilivu na kusameheana pale inapobidi ili kuwa na familia bora na imara.
" Tuwe wastahimilivu na tujue kusameheana sio wewe baba ukikosewa kidogo tu unachukua hatua ya kumpiga mama na wewe mama ukikosewa tu unachukua hatua ya kuchukua vitu vyako na kurudi kwa wazazi wako hiyo haipendezi, jua kuvumilia madhaifu ya mwenza wako" Amesema Ndemanga
Katika hatua nyingine, Mhe. Ndemanga amewaomba wananchi katika maadhimisho haya ya siku ya familia waitumie vyema kujadili mambo yanayohusu familia zao.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa