Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imetoa shilingi millioni 61 kwa ajili ya mikopo ya vijana, wanawake na walemavu kwa vikundi 28 vilivyopo Wilayani humo.
Hayo yamesemwa leo 24/07/2019 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo alipokuwa akiongea na wanavikundi hao katika ukumbi wa Rutesco mjini Ruangwa
katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa ndg, Andrea Chezue alisema huo siyo mwisho wa wanavikundi kupata mikopo hiyo, mwezi wa 8 mwaka huu Halmashauri itatoa million 100 kwa wanavikundi watakaoomba.
"Rudisheni kwa wakati marejesho yanayotakiwa muombe tena kwani fedha ziko za kutosha na zipo kwa ajili yenu ombeni kwa kufuata utaratibu mliowekewa nawahakikishi mtapata mikopo hiyo"
Ndg, Chezue alisema Halmashauri inaangalia uwezekano wa kuongeza fedha kwenye fungu la wanawake kwasababu wamekuwa wanarudisha kwa wakati marejesho yao na kundi lao limekuwa na uhitaji mkubwa kuliko makundi mengine.
Pia amewataka maafisa maendeleo ya kata na vijiji kuhamasisha watu wenye ulemavu kuunda vikundi vya ujasiliamali Ili waweze kujipatia mikopo ambayo inatengwa kwa ajili yao
"Sijafurahishwa na idadi ya kundi la watu wenye ulemavu ni vikundi vitatu tu ambayo vimepata fedha katika hiyo Milion 61 jitahidi sana huko kwenye kata na vijiji kutoa elimu kwa kundi hili wajue umuhimu wa hivi vikundi"
Aidha aliwatahadharisha wanavikundi wanaosubiri wagawane fedha alafu wavunje kikundi safari hii kutakuwa na ukaguzi wa kila baada ya mwezi 1, wataalamu wa Halmashauri watakuwa wanapitia kuangalia maendeleo ya kikundi hiko.
Alisema Mkurugenzi Chezue kikundi kinachoundwa na kinachosajiliwa kisife tunataka idadi ya watu waongezeke na si wapungue kikundi kitakachokiuka jambo hili kitajipunguzia nafasi ya kupata tena mkopo.
Ndg, Chezue aliwasisitiza wanavikundi kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwaahidi kuwawezesha watakao fanya mchakato huo.
Sambamba na hayo aliwahamasisha Wanawake kuchukua fomu za uchaguzi wa serikali za mitaa unaokaribia kutokana na wanawake kuwa makini katika mambo yao yote.
"Siyo kwamba kinababa hamko makini hapana mko makini pia ila kinamama nawao wachukie nafasi katika serikali za vijiji na kata ili kuwe na usawa wa majukumu kwa wanawake kwani wanaweza sana tu"
Naye bi, Emelda Chiwemba aliyeongea kwa niaba ya wanavikundi aliishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kuweza kuwapatia mikopo hiyo na pia aliwataka wanavikundi kuwa wabunifu zaidi na kuongeza ujuzi kupitia vikundi vingine.
Alisema bi, Emelda kusingekuwepo na huo utaratibu wa kukopeshwa na Halmashauri watu wengi wasingeweza kufanikiwa kama walivyofanikiwa sasa mikopo hiyo imetuinua zaidi.
"Mkurugenzi Chezue naomba nikuhakikishie tunaahidi kurejesha kwa wakati marejesho tunayotakiwa, nakuahidi hayatosua sua, kila mtu anataka arudishe apate nyingine kwa hili hatutokuangusha"
Pia amewataka wanakikundi kujifunza kupitia vikundi vingine ili waongeza ujuzi kufikia malengo ya kuwa na viwanda vidogo vidogo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa