Halmashauri ya WIlaya Ruangwa Mkoani Lindi kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Jamii imetoa tsh milioni hamsini na tano laki tatu na elfu hamsini (55,350,000/=) kuwakopesha vikundi vya vijana na wanawake wajasiliamali WIlayani humo kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.
Akizungumza katika ukumbi wa Rutesco WIlayani humo, kabla ya kukabdhi hundi hiyo kwa vikundi vya wajasiliamali, Mkuu wa Wilaya Ruangwa mh. Joseph Mkirikiti, amesema, pesa hizo zinatolewa ili jamii iweze kukuza uchumi na hivyo ni lazima kuzingatia masharti ikiwamo pamoja na kurudisha kwa wakati ili vikundi vingine viweze kupata nafasi ya kukopa .
Aidha amekemea juu ya tabia za watu wasioaminika kuchukua mkopo na kukwama kurudisha kwa wakati kuwa haifai kuwaacha na badala yake ameitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilayani humo kuwaelimisha wana vikundi vya ujasiliamali ili waweze kujua umuhimu wa kutumia fursa hiyo na kurudisha mkopo kwa wakati.
“Mnapochaguana chaguaneni watu mnaojuana vizuri, watu wasioaminika epukaneni nao, mikopo ni lazima irejeshwe na Yule asiekopesheka asikopeshwe” alisema Mkirikiti
Afisa Maendeleo ya jamii Wilayani Ruangwa bw. Rashidi Namkulala , amesema lengo kuu la kutoa mikopo hiyo ni kuwawezesha wajasiliamali waweze kuendesha shughuli zao wanazozifanya ili kuongeza kipato, huku akieleza kuwa mikopo hiyo imetokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri inayotengwa kutoka kwenye vyanzo mbali mbali kwa ajili ya kuwawezesha vikundi vya wajasiliamali.
Amesema hii ni awamu ya kwanza na kuwa awamu nyingine wanataegemea kutoa mikopo mwezi Mei na tayari vikundi vya wajasiliamali vimeshatuma maombi ya kutaka mikopo kupitia ofisi hiyo ya maendeleo ya jamii ambapo, wanategemea kuwapatatiwa mikopo hiyo mara baada ya utaratibu kukamilisha.
“Mpaka sasa hivi tumepokea maombi mengine ya vikundi ambayo imeomba mikopo mbayo tunatarajia mpka mwisho wa mwezi wa Mei tuwagawie hivyo vikundi vingine ambao wameomba mikopo” alisema Rashidi, ambae ni afisa maendeleo ya jamii WIlayani Ruangwa.
Nao wajasiliamali ambao ni wanufaika wa mkopo huo wameishukuru Halmashauri ya WIlaya Ruangwa kwa kuwawezesha kuwapatia mikopo hiyo huku wakiahidi kutumia kwa usahihi na kurudisha kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kukopa na kujikwamua kiuchumi.
Anusiata Cosmas ambae ni mjasiliamali kutokea kijiji cha Nandanga amesema kupatikana kwa mikopo hiyo ni nusura kwa vikundi vya wajasiliamali hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo vizuri huku akisisitiza kuwa kila mmoja anajua jinsi hali ya kiuchumi ilivyokua ngumu na hivyo unapopata fursa ni vizuri kuheshimu na kuitumia kama inavyopaswa.
“Tunashukuru sana Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, kwa kutupatia huu mkopo, huu mkopo utaenda kutusaidia zaidi kutuinua kiuchumi, maana hali ilikua sio nzuri kidogo kiuchumi lakini huu mkopo utaenda kutuwezesha kutuinua kidogo maana kuna miradi mingi ambayo tumeianzisha kma vile bustani, na kazi za ujasiliamali wa mikono”. Alisema anusiata.
Jumla ya vikundi 32 ambavyo 21 ni vikundi vya wanawake, vikundi 10 ni vijana na kikundi 1 ni walemavu, wanaojishughulisha na shughuli za ujasiliamali wa utengenezaji bidhaa, kama batiki, sabuni, vibegi, kulima bustani na mama lishe, wamepatiwa mkopo wilayani humo, ambapo kwa mujibu wa maelezo ya afisa wa maendeleo ya jamii wilayani ruangwa vikundi vingine vinavyoendelea kuomba mikopo hiyo watapatiwa mkopo mwezi wa tano mwaka huu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa