Katika kukabiliana na changamoto ya wanafunzi wa secondari wanaotokea vijiji vya michenga A, B na Mtawilile wwilayani Ruangwa mkoani Lindi, ambao wamekua wakitembea kwa Zaidi ya km 10 kuifikia shule ya sekondari Jirani, serikali kupitia mpango wa uboreshaji elimu ya sekondari imetoa fedha jumla ya shilingi milioni 560 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kijiji cha michenga.
Akitambulisha mradi huo wa ujenzi kwa wananchi wa kijii cha michenga Septemba 28 mwaka huu, kaimu mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa ambae pia ni afisa elimu secondary Mwl Ernest Haule, amesema mradi huo unapaswa kukamlika haraka ili mwaka wa wasomo 2024 wanafunzi waanze kujiunga na shule hiyo.
“Na lengo letu kubwa mwakani 2024 hiyo shule ianze na Watoto waanze masomo katika shule hiyo” alisisitiza Haule mbele ya wananchi wa Michenga.
Awali Diwani wa kata ya Malolo Mhe, Jafari Mwambe alibainisha miongoni mwa changamoto wanazopata Watoto wa Kijiji hicho ni kutembea umbali mrefu hadi kuifikia shule ya sekondari Jirani ya hawa mchopa ambapo wanafunzi hutembea km 9 hadi 10 na kubainisha kuwa sababu za msingi zilikuwapo michenga kupata shule ya sekondari kutokana na idadi kubwa nya wanafunzi wanaofaulu shule ya msingi kutoka katika vijiji hivyo.
“Wanatembea km 9 hadi 10 mpaka kuifikia shule ya sekondari ikiwamo Hawa mchopa na tuna sababu za msingi kuanisha shule za sekondari kwakua mwaka 2022 tulifaulisha jumla ya Watoto 95 ambao saw ana mikondo 2 ya madarasa ambao wote wanalazimika kutembea kuifika shule ya sekondari hawa mchopa” Alisema Mwambe.
Zaidi ya hekari 48 zimetolwa na wananchi wa Kijiji cha michenga ili kupisha ujenzi wa shule hiyo mpya itakayokua mkombozi kwa Watoto wao ambao baadhi yao wanatajwa kuishia njiani kutokana na umbali wa kuifika shule Jirani inayowalazimu kutembea Zaidi ya km 18 hadi 20 kwenda na kurudi.
Baadhi ya wazazi wakiwamo Makachila Ngitu, Safina Haji na Abdallah Chilumba wameeleza namna shule hiyo wanavoitegemea katika kutatua changamoto za Watoto wao na kubainisha utayari wao wa kushiriki kujitolea ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni Pamoja na kutoa maeneo kuchimba msingi na kushiriki katika ulinzi wakati ujenzi unaendelea ili vifaa vya ujenzi visiibiwe.
“Tunasukuru kupata mradi huu na tunaahidi kushiriki ujenzi wanafunzi wengi watasoma vizuri kwakua watakua wanaifika shule kwa karibu tofauti na ilivyokua awali” alisema Safina mmoja ya wazazi
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa