Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi amemtaka Afisa Elimu Msingi na Sekondari wa Wilaya Ya Ruangwa kuwachukulia hatua Waratibu elimu kata ambao awajatekeleza majukumu yao ya kwenda kukagua maandalio ya walimu katika shule zao husika.
Vilevile amewataka kuchukua hatua kwa walimu ambao awajaandaa maandalio hayo kama ambavyo muongozo wa masomo kwa muhula unavyomtaka.
Mkuu wa Mkoa aliyasema haya wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Ruangwa ukiwa ni muendelezo wa ziara alizozifanya katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa wa Lindi.
Mhe, Zambi alitoa maagizo hayo baada ya Kaimu Afisa Elimu Mkoa kukagua maandalio ya walimu katika shule ya Sekondari Ruangwa. Mbekenyera na Shule ya Msingi Likangala na kugundua udhaifu wa walimu kutokuandaa maandalio kama wanavyotakiwa.
Pia aliwataka walimu wa darasa la saba na kidato cha nne kuongeza juhudi katika kufundisha somo la kingereza kwa muda huu uliobaki wa wanafunzi kujiandaa na mtihani kwani katika somo hilo wako nyuma sana.
“Nimepita katika shule tofauti tofauti udhaifu niliougundua kwa watoto wa darasa la saba na kidato cha nne ni somo la kingereza linawashinda hivyo walimu mjitahidi sana katika kufundisha somo hili” alisema Mhe, Zambi.
Aidha Mhe, Zambi aliwausia wanafunzi kuacha kujiingiza katika masuala ya kimapenzi kwani umri wao bado mdogo na wanachotakiwa ni kusoma kwa bidii na si kuwazia mapenzi katika umri huo.
“Nyie bado ni watoto wadogo hayo mambo ya mapenzi mtayakuta wala msiyakimbili muda wenu ukifika mtayafanya mpaka mtachoka ila kwa kipindi hiki someni kwa bidii zote” alisema Mhe, Zambi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa