Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe, Shaibu Ndemanga aliyekuwa anamuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani, amewataka waendesha Pikipiki kujifunza alama za barabarani kwa umakini na kuzitumia kama ambavyo zinaelekezwa.
Mhe, Ndemanga aliwataka waendesha pikipiki wanavyoenda kujifunza kuandesha chombo hiko cha moto wanapaswa kuzingatia somo la alama barabarani kwani hii itasaidia sana kupunguza ajali
Mgeni Rasmi Mhe, Ndemaga aliyasema hayo katika siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani Kimkoa katika Wilaya ya Ruangwa iliyofanyika kuanzia 20/11/2017 hadi 24/11/2017.
Pia Mhe, Ndemaga alisisitizi suala la kujifunza alama za barabarani lisiwe ni la madereva tu wanaoendesha chombo hiko hata wananchi wanapaswa kujifunza na kuzielewa alama hizo ili kufanikiwa kupunguza ajali za barabarani.
“Lindi isiyo na jali za barabarani inawezekana na katika kufanikisha hili ni wajibu wa kila mwananchi wa Mkoa wa Lindi kujifunza umuhimu wa alama hizo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kwa ajali zinazotokea”alisema Ndemanga.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Lindi aliwataka waendesha pikipiki kwa ajili ya kujipatia riziki kuheshimu kazi hiyo na kuiona kama ni kazi nyingine kwani ndiyo sehemu inayowaingizia kipato na kufanya kuendesha maisha yao ya kila siku.
“Kazi mnayoifanya mnapaswa kuiheshimu kwa kiasi kikubwa kwani haina tofauti na kazi ya mtu anaenda ofisini kila siku asubuhi, nidhamu katika kazi yako ni chachu ya maendeleo” alisema Mhe, Ndemanga.
Vilevile Mgeni Rasmi aliwataka maafisa wa zimamoto kupita katika kila ofisi ya serikali kuangalia kama wanamifumo na vifaa vya kuzimia moto na ofisi itakayokosa vifaa hivyo basi mara moja iweke vifaa hivyo.
“Siyo tu maofisini hata katika taasisi zote za serikali kama shule na zahanati inapaswa ziwe na vifaa hivyo kwani hizi ni sehemu za mfano hata kwa jamii, wekeni vifaa vya zima moto katika maeneo hayo muhimu”alisema Ndemanga.
Pia Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kupunguza Umasikini na Kutunza Mazingira(APEC) Masalu Regu Rwandiko alitoa shukurani na kuiomba serikali kuendelea kuipatia ushirikiano taasisi hiyo inapofika katika Wilaya au Mmkoa kwa ajili ya kutoa huduma za elimu ya Usalama barabarani, elimu ya ujasiliamali na ulinzi shirikishi kwa waendesha pikipiki.
Masalu alisema kwa elimu wanayoitoa katika maeneo mbalimbali inasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali barabarani na kwa Wilaya ya Ruangwa ajali zimepungua kwa asilimia 76 .
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Joseph Mkirikiti aliwataka wakazi wa Ruangwa kutumia fursa zinazojitokeza kama ya kukopeswa pikipiki ambapo mkopeshwaji atapaswa kulipia kiasi cha fedha laki 4 za kitanzania kwa kuanzia alafu atapewa pikipiki hiyo na ataendelea kulipia kidogokidogo huku akiwa amekabidhiwa pikipiki yake
Aidha Mhe, Mkirikiti aliwataka vijana kuacha kukaa katika vijiwe muda wa kazi, fursa hizo zinajitokeza wanapaswa kuzipokea kwa mikono miwili na kuanza kufanya utekelezaji wake.
“Ikifika 2018 sitaki kuona vijiwe na nitavivunja mchana kweupe ndani ya Wilaya yangu sitaki watu wazembe na ndiyo maana nilipambana katika kuvunja vijiwe vyote vya (pull table) sasa ikifika huo mwaka nitamaliza vijiwe vyote vilivyobaki”alisema Mhe, Mkirikiti.
Mkuu wa Wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwakaribisha wananchi wa Mkoa Lindi na walio nje ya Lindi kuhudhuria katika sikukuu ya Maulidi ambayo kitaifa itafanyika katika Wilaya ya Ruangwa mkesha tarehe 30/11/2017 na sikukuu yenyewe itakuwa 1/12/2017.
“Karibuni tushereke siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W) tumejiandaa kupokea wageni kila mwenye nafasi anakaribishwa kujumuika na wanarungwa katika siku muhimu kama hiyo”alisema Mhe, Mkirikiti.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa