Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Hamisi Kigwangala ameuangiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kumalizia chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Mandawa kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia 06/10/2017.
Pia aliagiza kumaliziwa kwa chumba cha upasuaji cha Kituo cha Afya Mbekenyera kwa muda wa miezi 3 kwa kubadilisha vyumba vilivyokusudiwaa kwa wodi za wazazi kuwa jengo la upasuaji.
Mhe, Naibu Waziri aliyasema haya wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya ya Ruangwa tarehe 06/10/2017 alipotembelea vituoa vya Afya vilivyopo katika Wilaya hiyo ambavyo ni Kituo cha Afya cha Luchelegwa, Nkowe, Mbekenyera, na Mandawa pia alipata nafasi ya kutembelea zahanati ya Nandagala.
Naibu Waziri alisema katika utawala huu wa awamu ya tano ni lazima kila kituo cha Afya kiwe na chumba cha upasuaji, hivyo ni bora kuwa na chumba kidogo kuliko kukosekana kabisa chumba cha upasuaji.
“Mhe Mkuu wa Wilaya wewe hapa hauna vituo vya Afya una zahanati zenye majengo mengi vituo hivi vinamapungufu mengi ila ni lazima kuwepo na vyumba vya upasuaji ili kusaidia na kukidhi mahitaji ya wananchi” alisema Kigwangala.
Pia Naibu Waziri Kigwangala alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuwezesha kupatikana kwa maji katika vituo vyote vya afya vilivyopo katika wilaya hiyo alisisitiza kupatikana kwa maji katika hospitali kubwa na kubadilisha mabomba yaliyopo sasa katika vituo na hospitali ya wilaya.
Vile vile Naibu Waziri Kigagwala aliutaka uongozi wa hospital kufanya mchakato wa kufunga mfumo wa kielektroniki(GoT HOMIS) kwenye maeneo mengine na si kuishia mapokezi tu kama ilivyo sasa ili kudhibiti vyema mapato yanayoingia katika vituo hivyo na Hospitali ya Wilaya.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dr, Japhet Simeo alimuomba Mhe, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii na Jinsia Dr, Kigagwala awasaidie upatikanaji wa ramani rahisi zenye gharama nafuu kwa wananchi.
Dr, Simeo alisema ramani zilizoletwa Halmashauri zina na makadirio makubwa ya fedha ambayo kwa uhalisia utekelezaji wake unakuwa ni mgumu kwa wananchi.
“Sera ya sasa inawataka wananchi waanze kufanya shughuli za kimaendeleo kama ujenzi wa Zahanati mpaka kwenye boma alafu Halmashauri zimalizie ila kwa makisio ya fedha zinazokuwa zinaletwa inakuwa ngumu kwa wananchi kutekeleza Mhe, Kigagwala naomba suala hili ukatusaidie lipatiwe ufumbuzi kutokana na hali za wananchi wetu”alisema Dr, Simeo
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa