Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndg. Andrea chikongwe ametoa shukurani kwa shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG) na Mtandao wa jamii wa usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) kwa kuweza kutoa mafunzo ya uhifadhi wa misitu kupitia biashara endelevu za mazao ya Misitu katika kijiji cha Malolo.
Ametoa shukurani hizo wakati wa kikao kazi cha Ametoa shukurani hizo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha wadau wa misitu kinachotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa mpigo NMB kuanzia tarehe 6/2/22)
Mheshimiwa Chikongwe aliseme Malolo imepata bahati ya kupata elimu ya utunzaji msitu kwa kufanya shughuli ya uchomaji mkaa na uvunaji mbao wa misitu endelevu.
Kupitia mpango huo kijiji hiko kinategemea kupata shilingi million... katika shughuli za uvunaji mbao na uchomaji mbao kwa kufuata utaratibu kwa mpango wa utunzaji misitu.
"Natamani TFCG pamoja na MJUMITA kabla mradi huu aujaisha tuwe tumepata vijiji vingine vitakavyonufaika kama hiki cha Malolo uongozi utuangalie kwa jicho la karibu" amesema Chikongwe
Pia alisema Mashirika haya yamefanya jambo kubwa sana katika halmashauri ya wilaya ya ruangwa ambalo litasaidia kukuza uchumi wa kijiji na halmashauri.
"Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisiposhukuru tena MJUMITA NA TFCG imeleta jambo la maana sana katika wilaya yetu wanachotupatia ni bora zaidi kwani itakuwa ni elimu ya kurithishana" amesema Chikongwe
"Kijiji cha Ng'au na Malolo vilikuwa na mgogoro wa mipaka wa muda mrefu ambao ulionyesha dalili za usugu ila kupitia TFCG na MJUMITA wamemaliza mgogoro huo kabisa hii ni matunda ya mradi wa uhifadhi misitu wanaotupatia" amesema Chikongwe
Vile vile mheshimiwa Chikongwe aliwataka wafanyabiashara wa mazao ya misitu kufuata sheria katika kazi zao na kushirikiana ili kuhakikisha mapato ya vijiji husika na halmashauri hayapotei.
" Ni wajibu wa kila mtu kufuata sheria na kulinuda mapato ya halmashauri, twendeni tushirikiane ili tuweze kukusanya mapato ambayo yatawezesha na kusaidia kuongeza vijiji vingine katika mradi wa uhifadhi misitu, inawezekana tukawa na wilaya nzima iliyo katika mkakati wa kuhifadhi misitu. Mkaa endelevu rafiki wa msitu, mbao endelevu rafiki wa msitu" amesema Chikongwe.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa