Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo Ruangwa ndg, Frank Chonya amewataka mawakala wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria kama zilivyoainishwa na tume ya uchaguzi.
vile vile Aliwasihi kutofanya zoezi la uwakala kwa mazoea kwa kuwa ni zoezi muhimu ambalo linaitaji umakini na uaminifu mkubwa
Amesema hayo wakati wa zoezi la kuwaapisha Mawakala hao leo tarehe 21/10/2020 mjini Ruangwa.
Pia amewataka kuzingatia matakwa ya katiba, sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi na si kufuata matashi (hisia/itikadi) yao katika kusimamia kazi ya uwakala.
“Vyama vimewateua nyie kwa sababu vina waamini na vina imani mnaweza mmkutekeleza maelekezo ya tume yanayo wataka mzingatie ifikapo tarehe 28/10/2020” amesema Chonya.
Alisema Msimamizi wa uchaguzi Chonya "nendeni mkasimamie amani na si kuwa chanzo cha kuvuruga amani". Aliwasisitiza wajitahidi kuzingatia misingi na maelekezo ya tume katika shughuli zao ili kuepusha taharuki kwa wagombea wao.
“Kasomeni vitabu mlivyopewa ili kutambua kazi mtafayoifanya. Vitabu hivyo ndiyo muongozo wenu na si kitu kingine chochote” amesema Chonya
Jumla ya mawakala 1,012 wa nyama vya siasa vyote wameapishwa leo Wilaya Ruangwa.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa