• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

MATOKEO YA SENSA YAWAFIKIE WATENDAJI WOTE WA MIKOA NA HALMASHAURI

Posted on: July 2nd, 2024

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema matokeo ya sensa yanapaswa yawafikie watendaji na walengwa wote katika ngazi ya mkoa na Halmashauri na yawe msingi wa rejea katika kufanya maamuzi yote ya kibajeti, kupanga miradi ya maendeleo na kufuatilia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kisekta.


Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Julai 2, 2024) wakati akizungumza na viongozi, wananchi na wadau mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Halmashari za Wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi uliofanyika kwenye viwanja vya Maonesho, Kilimahewa mjini Ruangwa.


Amesema usambazaji na mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa viwe ni ajenda ya kudumu katika vikao vyote vya kikanuni katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri. “Watendaji wote myabebe haya matokeo mkayatumie, muwe viongozi wa kuhakikisha yanatumika.”


Amewataka viongozi na watendaji wakae pamoja na kutafakari namna bora ambayo matokeo ya sensa yanaweza kutumika kubadili hali za maisha ya wananchi pamoja na kuhimiza uwekezaji. “Matokeo haya yanapaswa yatumike na yasaidie kubadilisha maisha ya wananchi huku mkijua kwamba fedha nyingi zimetumika kuifanya kazi hiyo,” amesema.


Akitolea mfano Mkoa wa Lindi, Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa amesema: “Mkoa wa Lindi una fursa nyingi za kuvutia uwekezaji hivyo ni wakati sasa wa kutumia matokeo haya ya sensa kuitangaza Lindi na kuibadili kupitia uwekezaji.”


Amewataka viongozi hao waifanye kazi ya kuhuisha anwani za makazi na kuweka mikakati ya kutunza miundombinu yake kuwa ni endelevu kwa ajili ya kurahisisha ufikiwaji wa wananchi, kurahisisha biashara mtandao, uwekezaji na uwajibikaji. “Kila Halmashauri nchini, ifanye uhakiki wa vibao vilivyowekwa, waelimisheni wananchi umuhimu wake na pia wasiving’oe kwa sababu vinasaidia kuelekeza hata akija mgeni kwa mara ya kwanza hahitaji kuelekezwa na mtu au kuulizia kwa mtu anakokwenda,” amesisitiza.


 Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande alisema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwenye ufanyaji wa sensa ya watu na makazi kwa njia ya kidijitali.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa