Mkuu wa Wilaya ya Mhe. Ruangwa Hashim Mgandilwa amepiga marufuku wamiliki wa viwanja vya kucheza unyago kutumia Mangariba wasio na vitambulisho vya mjasiliamali mdogo.
Amesema hayo leo Mei 23/2019 wakati wa kikao cha mangariba, waganga wajadi na wamiliki wa viwanja vya kuchezea unyago kilichofanyika ukumbi wa CCM Ruangwa mjini.
Pia amewataka waganga wa jadi kuwa na kitambulisho cha mjasiliamali mdogo kama wanataka kuendelea kutoa tiba katika Wilaya ya Ruangwa.
Mheshimiwa Mgandilwa amewataka wamiliki wa viwanja kuzingatia ratiba ya kufunga na kufungua shule ili mtoto anaechezwa unyago asikose haki ya kupata elimu.
"Msitafute shida Halmashauri ikianza kutoa vibali vya sherehe hizo nìtafuatilia kama umepokea watoto siku husika ya tarehe 8 mwezi wa 6 na kumaliza tarehe 6 mwezi wa 7 ikifika tarehe ya mwisho watoto wote wawe wametoka"
Mkuu wa Wilaya amewataka kuhakikisha watoto wanapokuwa jandoni wanalazwa kwenye chandarua kuepusha maradhi na kuzingatia usafi wa maeneo ya viwanja.
"shughuli hizi zingatieni msingi ya afya kila mwenye kiwanja awe na uhakika na daktari ni vyema tukaangalia usalama wa watoto wetu" DC Mgandilwa
vile vile amewataka kuzingatia mafunzo wanayotoa kwenye jando na unyago yaendane na maadili ya kitanzania na umri wa watoto wanaopewa hayo mafunzo.
Mkuu wa Wilaya ya Mhe. Ruangwa Hashim Mgandilwa amepiga marufuku watu wenye viwanja vya kucheza unyago kutumia Mangariba wasio na vitambulisho vya mjasiliamali mdogo
Amesema hayo leo Mei 23/2019 wakati wa kikao cha mangariba, waganga wajadi na wamiliki viwanja vya kuchezea unyago kilichofanyika ukumbi wa CCM Ruangwa mjini.
Pia amewataka waganga wa jadi kuwa na kitambulisho cha mjasiliamali mdogo kama wanataka kuendelea kutoa tiba katika Wilaya ya Ruangwa.
Mheshimiwa Mgandilwa amewataka wamiliki wa viwanja kuzingatia ratiba ya kufunga na kufungua shule ili mtoto anaechezwa unyago asikose haki ya kupata elimu.
"Msitafute shida Halmashauri ikianza kutoa vibali vya sherehe hizo nìtafuatilia kama umepokea watoto siku husika ya tarehe 8 mwezi wa 6 na kumaliza tarehe 6 mwezi wa 7 ikifika tarehe ya mwisho watoto wote wawe wametoka"
Mkuu wa Wilaya amewataka kuhakikisha watoto wanapokuwa jandoni wanalazwa kwenye chandalua kuepusha maradhi na kuzingatia usafi wa maeneo ya viwanja.
"shughuli hizi zingatieni msingi ya afya kila mwenye kiwanja awe na uhakika na daktari ni vyema tukaangalia usalama wa watoto wetu" DC Mgandilwa
vile vile amewataka kuzingatia mafunzo wanayotoa kwenye jando na unyago yaendane na maadili ya kitanzania na umri wa watoto wanaopewa hayo mafunzo.
Pia alisema watazingatia sheria zilizoweka na watakumbushana pale mmoja wao anapotaka kuvunja makubaliano hayo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa