Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ameyataka majeshi yote nchini kusambaza maarifa ya kilimo bora kwa jamii inayowazunguka. amesema huu ni muda muafaka kwani taifa linapopanga kupiga hatua kuelekea Uchumi wa viwanda ni budi kuhakikisha jamii nzima inashirikishwa kwa kupata maarifa ya teknolojia mpya.
Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo wakati akifungua maonesho ya Nanenane Kitaifa yaliyofanyika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo. Amesema taifa linapokuwa halipo vitani, inatarajiwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kuwekeza katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali na hata kuisadia jamii kufikia malengo. Badala ya hali kuwa hivyo badala yake imekuwa ni jambo la kawaida kwa maeneo ya Jeshi kuwa na uzalishaji wenye tija kwa mazao ya aina mbalimbali lakini jamii inayowazunguka ikiwa duni.
Amesema jambo hili halikubaliki na kwamba jeshi la wananchi linatakuwa kuwa rafiki wa jamii inayowazunguka. Liweke miundmombinu na mkakati imara wa kuhakiksiha jamii inaiga na kuzalisha kama wao wanavyozalsiha na kwamba hilo si suala la kusubiri jamii iwafuate bali mipango ya jeshi ielekeze huko.
Mheshimiwa Simbachawene ambaye aliridhishwa na ubora wa mabanda ya maonesho ya jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa jinsi walivyopiga hatua kubwa katika uzalishaji amesema hilo ni jambo la kujivunia na kwamba haya yote yanatokana na nidhamu kubwa ya na uamuzi wa dhati wa kuwekeza katika masuala hayo lakini haikubaliki katika jamii iwapo uwezo huo unaishia kwa jeshi tu wakati jamii inayozunguka wanaishi kwa shida na hawana maarifa yoyote ya uzalishaji.
Awali akielezea uzalishaji uliowekezwa na jeshi hilo, Luteni kanali Peter Lushika wa Suma JKT amesema Jeshi limejipanga na limekuwa likitengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo, viatu na mazao ya kilimo. Pia limekuwa likitoa mafunzo mbalimbali ya uzalishaji bora kwa vijana.
Ametoa wito kwa aserikali kuendelea na msisitizo wa kuwataka wananchi wa Tanzania kutumia na kupenda bidhaa za ndani ili kuinua wazalishaji wa ndani.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego amesema Jeshi la wananchi wa Tanzania Limejipanga lakini bado linapaswa kuhakikisha jamii inaondoa woga wa kupata maarifa kutoka kwa maaskari. Amesema zama za wananchi kuogopa maaskari zimekwisha hivyo jeshi lijipange lihakikishe liko karibu na wananchi. Liweke mazingira ambayo yatawafanya wananchi wawe huru kujifunza kutoka jeshini na hivyo kuwa na mabadiliko ya pamoja kimaendeleo.
Maonesho ya Wakulima Kitaifa maarufu kama Nanenane yamefunguliwa Leo katika viwanja vya Ngongo vilivyoko katika halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi. KauliMbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni “Zalisha kwa tija mazao ya Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa Kati.
Maonesho haya ya siku nane yanatarajiwa kufungwa Agosti nane ambapo Mgeni Rasmi natarajwia kuwa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa