Ikiwa ni katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini yenye kauli mbiu zama za mapinduzi ya nne ya viwanda safari ya maboresho kuelekea mahakama mtandao Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ruangwa, Mh. Mariam Omary Machomba, amesema kuanzishwa kwa huduma hiyo kutasaidia kuharakisha kuamuliwa kwa mashauri mbalimbali na kusisitiza wananchi kushirikiana na mahakama kwa kutoa mrejesho kuhusu huduma mbali mbali zinazotolewa kupitia simu janja.
Akibainisha zaidi mbele ya wadau wa sheria na wananchi waliohudhuria hafla hiyo ya kilele cha siku ya sheria iliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya mahakama ya wilaya, Mhe. Mariam ameeleza mahakama mtandao itasaidia kuondoa wasi wasi ama hofu kwa wateja kwakuwa wanaweza kutoa taarifa zao za malalamiko kwa njia ya simu nambari 0752 500 400 jambo litakalosaidia kufahamu taarifa za shauri la mteja husika bila kulazimika kuwepo mahakamani mara zote.
‘Sasa hivi malalamiko unapiga tu simu ukiwa huko huko kijijini kwako na lalamiko linapokelewa na kwenda moja kwa moja bila kuhofia kama Hakimu hatapokea na kufanyia kazi kwani kuna kitengo maalumu cha malalamiko watapokea simu hii na kufanyia kazi, alisema Mh. Mariam.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mhe. HASSAN NASOR NGOMA ametoa rai kwa watendaji wa mahakama kuhakikisha wanajiridhisha katika mfumo wa matumizi ya njia hiyo ya mtandao ili kuepuka changamoto mbali mbali za kimtandao ikiwa ni pamoja na kudukuliwa kwa taarifa nyeti, na kuwataka wahusika katika muhimili huo kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya namna sahihi ya kutumia ikiwa ni pamoja na kuzingatia na ubora wa mitandao husika.
Wiki ya sheria nchini ilianza januari 23 mwaka huu ambapo maadhimisho yake yamefanyika Februari 2, mikoa na wilaya mbali mbali imeazimisha huku kitaifa ikifanyika katika viwanja vya chinangali park mkoani DODOMA
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa