Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na wakuu wa idara wamezindua program ya kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.
Yusta bonface Akiwasilisha mada mbele ya Madiwani na wakuu wa Idara mratibu wa program hiyo ngazi ya mkoa bwana Yustaki Boniface katika ukumbi wa Rutesco hapa Ruangwa amesema kuwa Lengo la program hiyo kuongeza faida za kichumi,kijamii na kimazingira na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu.
Vilevile Yusta amesema Programu hii inatekelezwa mkoani lindi katika wilaya za Ruangwa,Nachingwe na Liwale chini ya ufadhili wa serikali ya Finland
Amesema Serikali ya Tanzania imetoa fedha kiasi cha Tsh milioni 500 na Serikali ya Finland imechangia sh bilioni 9.95
Kwa wilaya ya Ruangwa Program itaanza katika kata 10 na vijiji 10 ambazo ni Mbwemkuru kijiji cha Machanganya,kata ya nandagala kijiji cha Mmawa,kata ya Nambilanje kijiji cha Mtondo,Kata ya Mandarawe kijiji cha Nandenje,Kata ya Likunja kijiji cha Kitandi,Kata ya Malolo kijji cha Michenga,Kata ya Mandawa kijiji cha Nahanga,Kata ya Mnacho kijiji cha Ngau,Kata ya Chibula kijiji cha Lichwachwa na kata ya Mbekenyera kijiji cha Chingumbwa
Naye Mkuu wa idara ya Ardhi na Maliasili anafafanua zaidi kuwa mradi huu utafika mpaka kwenye kata 11 zilizobaki kabla ya kumalizika kwa mradi huo.
"Waheshimiwa Madiwani msiwe na wasiwasi huu mradi utafika katika maeneo yote ya Kata ya Ruangwa kabla aujaisha wananchi watanufaika na wanakijiji watanufaika" amesema Masangya
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa