Madiwani wa Kata mbalimbali wilayani Ruangwa wamewasilisha taarifa zao za utekelezaji katika kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2023/2024 katika Mkutano wa baraza la Madiwani uliofanyika leo Mei 20, 2024 katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa.
Mkutano huo umehusisha Madiwani wa Kata zote, Watendaji wa Kata na Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na taarifa ya idadi ya watu, hali ya kiusalama, hali ya upatikanaji wa chakula, hali ya ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hali ya majanga katika Wilaya ya Ruangwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ambaye ni Diwani wa Kata ya Nandagala Mhe. Andrew Chikongwe amewataka TARURA kufanya marekebisho ya miundombinu ambayo imeharibiwa na mvua ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kuelekea kipindi hiki cha misimu.
Aidha, Mhe. Chikongwe ametoa wito kwa Madiwani kila mmoja kwa nafasi yake kuzungumzia Mwenge wa Uhuru na faida zake kwa wananchi ili wahamasike na waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za na sherehe za Mwenge.
"Tunaweza kuwa namba moja katika mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwani mwaka uliopita katika Halmashauri za Mikoa mitano Kanda ya Mashariki, Ruangwa tumekuwa wa kwanza sasa twendeni tukahamasishane wote ili tuweze kuwa wa kwanza Kitaifa na inawezekana" Amesema Chikongwe.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa