Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi amweataka madiwani wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanatengeza mpango kazi na mikakati Madhubuti ya kulipa madeni mbali mbali inayodaiwa halmashauri hiyo ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuharakisha shughuli za maendeleo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia taarifa ya baraza la madiwani la hesabu za mwaka 2020/21 na 21/22 iliofanyika septemba 29, 2022 katika ukumbi wa mkuu wa wilaya, taarifa zilizonyesha kuwapo kwa madeni kadhaa inayodaiwa halmashauri hiyo na watumishi ambapo amesema kulipa kwa madeni hayo kutarahisisha shughuli za kimaendeleo Kwenda kwa kasi kutokana na watumishi hao kutokua na kinyongo na serikali yao.
“Maombi yangu ni kwamba Madiwani tutengeneza mpango wa namna ya kupunguza madeni ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi” alisema Ngoma.
Awali muweka hazina wa halamshauri Saidi Jabali alieleza kuwa kumekua na ufanisi katika matumizi sahihi ya fedha ikilinganishwa mwaka 2020/21 na 2021/22 kwaku katika mwaka 2021/22 pamokja na kuwa na kiasi kikubwa na miradi mingi lakini matumizi yamekua makubwa kama ilivyopaswa huku akiseama mwaka 20/21 palikua na pesa kidogo lakini bado haikutumika ipasavyo kiasi kupelekea kubaki kwa salio kubwa.
“ukilinganisha na mwaka jana utaona kwamba mwaka jana tulifunga hesabu kwa fedha taslimu Shilingi Bilioni mbili na milioni ishirini na nne, lakini mwaka huu tumefunga fedh Taslimu shilingi Bilioni moja na milioni mia tano kumi na sita, hii inamaanisha kuwa kuna ufanisi mkubwa wa matumizi ya fedha tumeongeza” alisema Saidi.
Kwaupande wake Prosper Roman ambae ni katibu tawala msaidizi mkoa wa Lindi nae alitumia wasaa wa kikao hicho kumuhimiza muweka hazina kuwahisha vitabu vya mahesabu kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ili kukamilisha ufungaji wa mahesabu hayo, huku baadhi ya madiwani wakiwamo Rajabu Macholilo na Daniel Chilemba wakieleza namna walivyoridhika na mwenendo wa matumizi na vipaumbele katika manedeleo ya Halmashauri hiyo kwa kueleza kuwa wanaona safari ya maendeleo ikikua kwa kasi kutokana na mpango sahihi wa matumizi ya fedha.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa