Kutokana na kuongezeka changamoto ya vifungashio vya zao la korosho kwa wakulima kutokuwafikia kwa wakati jambo linalopelekea kuchelewa kwao kuzifikisha korosho katika magahala makuu ili kuuza, Baraza la madiwani Halmashaauri ya wilaya Ruangwa limemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuchukua hatua za kuhakikisha Halmashauri inanunua magunia.
Agizo hilo limetolewa leo tarehe 28/11/2019 wakati wa kikao cha baraza la robo kilichofanyika katika ukumbi wa Rutesco Ruangwa mjini.
Baraza hilo limemtaka Mkurugenzi kuwahi ununuzi wa magunia hayo ili kuwahi kunusuru korosho za wakulima ambazo zinaelezwa wenda zikapoteza ubora kutokana na kutunza katika maeneo yasio na sifa.
Wakichangia hoja baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao hicho cha Baraza la Halmashauri ya Wilayani humo wamemtaka mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kupitisha maamuzi ya kupata vifungashio ili kukomboa wakulima wa zao hilo kwani wananchi wengi wamekua wakilalamikia tatizo hilo.
“Tunakosa pakuwek sura zetu huko katika maeneo yetu wananchi awatuelewi kwasababu ya korosho zao kutokwenda katika ghala kubwa kwa kukosa vifungashio Mkurugenzi tunaamini agizo hili utakifanyia kazi kwa uharaka zaid”Diwani Chikongwe
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri wilaya ya Ruangwa Rashidi Nakumbya alimtaka aliitaka bodi inayoendesha ghala kuhakikisha kororsho zinatoka katika maghala ya vijiji na kufika katika ghala kubwa la mjini.
“Vifungashio vikifika katika maghala ya vijini hakikisheni korosho inakuja katika ghala kubwa kwa uharaka ili kuwahi minada inayofuata” Nakumbya
Inaelezwa katika wilaya ya Ruanagwa mategemeo ni kukusanya tan 13,000/= za korosho lakini mpaka sasa zimekusanywa tani 3,700 kutokana na uhaba wa magunia ya kufungashia korosho kutoka kwa wakulima na vyama vya msingi jambo linalohofiwa wenda likaleta hasara kubwa kwa wakulima na vyama vya msingi ikiwa ni pamoja na halmashauri kukosa mapato yake.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa