Halimashauri ya wilaya ya Ruangwa imekabidhi pikipiki nne Kwa maafsa ugani ili ziwasaidie katika shughuli za ugani wilayan hapo
Akikabidhi pikipiki hizo mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Ruangwa Mh Andrew Chikongwe Leo wakiwa katika halimashauri hiyo amewataka maafisa ugani hao kutunza vyombo hivyo kwani jamii inahitaji kufikiwa na wataalamu hao huko mashambani ili kutoa huduma za ugani Kwa wakulima.
Akizungumza baada ya kupokea pikipiki hizo mkuu wa idara ya kilimo Bw.Nolasco Damiani Kilumile amesema pikipiki hizo nne zenye zaidi ya thamani ya shilingi million 10 wamezipokea kutoka bodi ya korosho zikiwa na lengo la kusaidia maafisa kilimo katika shughul za ugani kupitia wataalamu ili kuongeza tija katika zao la korosho nchini , ikiwa pikipiki hizo zimetolewa Kwa maafsa ugani wa kata tatu chinongwe,mandawa pamoja na makanjiro.
Naye mratibu wa zao la korosho wilaya ya ruangwa Richard Bendera ambae ni mmojawapo ya wataalam waliopokea pikipiki hizo amesema zitawasaidia kuwafikia wakulima katika kusimamia usambazaji wa pembejeo kwa wakulima kutoka katika ghala kuu ,kukuza ubanguaji mdogo na wakati pamoja na kukuza soko la ndani na la nje ya nchi Kwa kusimamia minadai na mauzo mbalimbali ya korosho yanayofanyika katika maeneo tofauti tofauti.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa