MAAFISA Lishe kutoka Hospitali ya Wilaya ya Rungwa naKituo cha Afya Ruangwa Mjini, leo Novemba 06, 2025 wametoa elimu ya lishe kwa watumishi wa Halmashauri yaWilaya ya Ruangwa, ikiwa ni sehemu ya kampeniendelevu ya kuhamasisha ulaji bora na afya njema kwawatumishi wa umma.
Elimu hiyo imetolewa katika ukumbi wa Halmashauri yaWilaya ya Ruangwa, ikilenga kuwajengea watumishiuelewa mpana kuhusu umuhimu wa mlo kamili, ulajiunaozingatia makundi yote ya chakula, na namna lishebora inavyoweza kuongeza ufanisi na tija katika utendajiwa kazi za kila siku.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Lishe kutokaHospitali ya Wilaya ya Rungwa, Bi. Martha Theophil,amesema changamoto kubwa inayowakabili watumishiwengi ni kutopata muda wa kula chakula sahihi kutokanana majukumu mengi ya kazi, jambo linalochangiakuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari na unene uliopitiliza.
Kwa upande wake, Afisa Lishe kutoka Kituo cha AfyaRuangwa Mjini, Bi. Luciana Joseph amewataka watumishikuzingatia matumizi ya vyakula vya asili vinavyopatikanakatika maeneo yao, hususan mboga mbichi, matunda, nafaka zisizokobolewa na protini za mimea na wanyama, badala ya kutegemea vyakula vya viwandani ambavyohavina virutubishi vya kutosha.
Aidha, Maafisa hao walisisitiza umuhimu wa kufanyamazoezi mara kwa mara, kunywa maji ya kutosha, nakupunguza matumizi ya chumvi, mafuta na sukari kupitakiasi, wakibainisha kuwa tabia hizo ndogo za kiafya zinamchango mkubwa katika kujikinga na magonjwa sugu.
Watumishi wa Halmashauri walioshiriki mafunzo hayowalieleza kufurahishwa na elimu waliyopata, wakisemaimekuwa ni fursa muhimu ya kujitathmini kuhusumwenendo wao wa ulaji na kujipanga upya kuboreshaafya zao kwa manufaa binafsi na ya taasisiwanazozitumikia, huku wakipata fursa pia ya kuulizamaswali mbalimbali.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za Halmashauri yaWilaya ya Ruangwa katika kuboresha afya za watumishiwake, ili kuongeza ari, tija na ufanisi kazini kupitiamwamko mpya wa lishe bora na maisha yenye afyanjema.
Mbali na mafunzo, Maafisa hao walitoa huduma yaUpimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa watumishiwote waliojitokeza kushiriki, ikiwemo Shinikizo la Damu(Presha) pamoja na Uzito.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa