Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe Hashim Mgandilwa ameagiza kamati ya ujenzi wa zahanati ya Namungo na kamati ya wazee kulipa mabati 28 yenye thamani ya fedha shilingi 78,4000 mpaka tarehe 10/07/2019 ambayo hayajulikani yalipo.
Ametoa agizo hilo tarehe 26/06/2019 wakati wa mkutano wa kusomewa mapato na matumizi ya fedha zilizochangwa na wananchi wa eneo hilo kwa lengo la ujenzi wa zahanati katika kitongoji cha Namungo.
Mheshimiwa Mgandilwa alisema kitengo cha bati hizo kutokuonekana na kutokujulikana zilipo ni uzembe wa kamati na kukosekana kwa umakini kwa watu hao.
" Mlichofanya ni uzembe wa mali ya umma nawapeni wiki mbili tu kuanzia tarehe ya jana mrudishe hiko kilichopotea, rudisheni fedha ili ziendele kutumika katika ujenzi wa zahanati hiyo" amesema Mgandilwa
Mkuu wa Wilaya aliwaambia wanakamati hizo suala la kuwalipisha bati hizi si kutaka kuwakomoa ni kutaka kuwajenga ili wawe makini na mali za umma na kutimiza wajibu wao katika majukumu wanayokabidhiwa na wananchi.
Pia ameagiza kuwe na kamati ya fedha ya Namungo ili wao ndiyo wawe wasimamizi wa fedha zao na itakayofuata taratibu na sheria zote za utunzaji na utoaji fedha ili kuwe na njia salama ya utoaji fedha
"Mnamatumzi mengi kuliko hata makusanyo na matumizi mengi yanamashaka kwasababu utaratibu wenu wa utoaji wa fedha si rafiki undeni kamati ya fedha ulizeni serikali ya kijiji wanafanyaje mpaka wanapata kamati na kamati hiyo inamajukumu gani"
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa