Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa ametekeleza agizo la Mheshimiwa Rias John Pombe Magufuli kwa vitendo alilomtaka kuhakikisha yanapatikana madawati ya kutosha kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Likunja iliopo wilaya humo mpaka kufika saa sita ya leo octoba 16.
Mheshimiwa Mgandilwa ametekeleza agizo hilo kufuatia ziara ya Mhe. Magufuli hapo jana alipotembelea Wilayani Ruangwa jana na kusimama katika kijiji cha likunja na kuzungumza na wanafunzi na kusikiiza kero zao ndipo wakataja upungufu wa madawati kwa kidato cha kwanza.
Mkuu wa Wilaya amekabidhi viti na madawati 100 kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Likunja leo tarehe 16/10/2019 Ruangwa mjini.
“Tushirikiane kujenga Ruangwa yetu kama kuna changamoto huko zileteni katika ofisi husika tuzifanyie kazi mapema kwa lengo la kuwa Na Ruangwa bora na isiyo na changamoto ndogo ndogo kama hizi za madawati” amesema Mgandilwa
Naye Afisa Elimu Sekondari Wilayani humo Ernest Haule ameeleza kuhusu kuwapo kwa upungufu wa madawati kwa baadhi ya shule Wilayani humo huku akikiri kuwa upatikanaji wa madawati hayo ni msaada mkubwa kwa shule hiyo.
Ndg,Haule ailiishukuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwapatia madawati hayo katika shule ya Sekondari Likunja kwasababu ilikuwa inauhitaji mkubwa wa madawati hasaa kwa kidato cha kwanza na pili ambao watakuwa wanufaika wa msaada
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ya Likunja wameeleza furaha yao ya kupatiwa madawati hayo na kushukuru ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kutimiza ahadi hiyo kwa wakati.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa