Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndugu Godfrey Mnzava aweka jiwe la Msingi katika Mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji uliopo katika kijiji cha Nandagala Tarafa ya Mnacho Wilaya ya Ruangwa leo Mei 28, 2024 ambao umegharimu zaidi ya Bilioni 1.6 za Kitanzania.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kulinda na kutunza vyanzo vya maji ili kuendelea kupata maji safi na salama kama ilivyo jitihada ya Serikali kuhakikisha wananchi wanapata maji na salama na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti.
Katika hatua nyingine amewapongeza RUWASA kwa kutumia vyema mfumo wa usimamizi wa manunuzi ya Umma.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa