Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndugu Godfrey Mnzava ameweka jiwe la Msingi Kituo cha Afya kilichopo kijiji cha Nangumbu Kata ya Malolo wilayani Ruangwa kilichogharimu shilingi Milioni 324 za Kitanzania.
Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 28, 2024 ambapo kituo hicho kimejengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na ni kutokana na kutambua umuhimu wa uwepo wa huduma za Afya karibu na wananchi.
Aidha, Ndugu Mnzava atoa wiki mbili kwa wataalamu wa kudhibiti Malaria Wilaya ya Ruangwa kuhakikisha dawa za viuwa wadudu wanaosambaza Malaria zinapatikana na kupuliza kwenye maeneo ya mazalia ya mbu ili kutokemeza Malaria Tanzania kufuatia ujumbe wa Serikali" Ziro Malaria inaanza na mimi, nachukua hatua kuitokomoza"
Katika hatua nyingine, Mnzava ashiriki katika zoezi la upandaji wa miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa