Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa ndg, Fabian Chonya amekabidhi magari manne kwa idara ya Mipango, Fedha, Elimu na Ujenzi.
Amekabidhi magari hayo tarehe 02/10/2020 katika ofisi ya Mkurugenzi Ruangwa Mjini.
Mkurugenzi Chonya amewataka wakuu wa idara waliokabidhiwa magari hayo kuyatumia kusimamia shughuli za maendeleo zinazofanyika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ruangwa.
“Afisa mipango gari hilo litumike katika kusimamia miradi tunayoitekeleza iliyo mjini Ruangwa na nje ya Ruangwa ninaimani mtalitumia katika kusimamia vizuri miradi hiyo” amesema Chonya
Aidha alisema ndg, Chonya kuwa gari hizo zisitumike tu na wakuu wa idara au watu waliokabidhiwa pekee na kwamba mtumishi yoyote anayekwenda kutekeleza shughuli za kiofisi anapaswa kutumia gari hizo.
“Mtumishi yoyote unataka kwenda mjini kutekeleza shughuli ya kiofisi nenda kaombe gari kwa muhusika na ulitumie sitaki kuona unatumia pikipiki kutekeleza shughuli za kiofisi haya ni magari yenu wote” amesema Chonya
Vilevile Mkuu wa idara ya Elimu Msingi ndg, Suleimani Mrope amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwapatia magari hayo kwani yatarahisisha kufanya shughuli za elimu ambazo mwanzo zilikuwa ngumu kuzifikia kutokana na kukosekana usafiri.
Alisema Mwalimu Mrope kuwa amefanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa miaka 9 na hajawahi kutokea wakuu wa idara wakakabidhiwa magari na mkurugenzi mbele ya watumishi wote kama ilivyofanyika leo.
“Kwa hili Mkurugenzi nashukuru sana kwa niaba watumishi wa wote na niwatoe hofu watumishi wa chini yetu kuwa haya ni magari ni ya Halmashauri na si ya mtu binafsi au la idara fulani hivyo kama una kazi ya kiofisi usisite kuomba gari tutashirikiana katika kutekeleza shughuli za Halmashauri.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa