WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. milioni 250 kwa ajili ya usambazaji wa huduma ya maji safi katika kijiji cha Chimbila ‘B’ kichopo kata ya Mnacho.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mnacho wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi wilayani hapa.
Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji, ambapo itahakikisha wananchi wanapata huduma hiyo katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Amesema mbali ya maji kusambazwa kwa wananchi, pia yatasambazwa kwenye taasisi zote za umma zikiwemo shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea shule ya Sekondari ya Mnacho na kuzungumza na wanafunzi, ambapo amesema Serikali inatarajia kujenga mabweni mawili katika shule hiyo ili wanafunzi waweze kuishi shuleni na kupata fursa nzuri ya kujisomea.
Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya wanafunzi wa kike shuleni hapo kuiomba Serikali iwajengee mabweni ili waweze kuishi shuleni na kupata muda mwingi wa kujisomea.
Wanafunzi hao wamemueleza Waziri Mkuu kwamba kitendo cha kuishi nyumba kinawakosesha muda wa kujisomea kwa sababu ya hupangiwa kazi nyingi wanapofika nyumbani, hivyo kukosa muda wa kujisomea.
(Mwisho)
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa