Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Elimu Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg. Vicent Kayombo ameitaka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kumaliza miradi yote ya shule shikizi kufikia tarehe 19/03/2019 pamoja na miradi yote ya maboma katika shule za sekondari kufikia 19/04/2019 kwani shule hizo zimeishapokea fedha tangu tarehe 19 Februari 2019.
Ndg Kayombo ameyasema hayo siku ya tarehe 11/03/2019 wakati wa kikao kazi cha utekelekezaji wa miradi ya Elimu kwa Walimu wakuu, Wakuu wa shule, Waratibu Elimu Kata, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji pamoja na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri.
Akiwa katika kikao hicho Ndg Kayombo amewataka viongozi wote kutotumia fedha za miradi zinazoletwa kulipana posho, pamoja na kwenda kutimiza wajibu wao kwenye maeneo yao ili kukamilisha miradi hiyo kabla kabla ya kupita kukagua kwa awamu nyingine .
"Tusije kulaumiana nikikuta jambo kama hili sitoweza kulivumilia hizo ni fedha za ujenzi na zinakuja na maelekezo yake maalum sasa mnaolipana posho kwa fedha hizo tusijekulaumiana"amesema Kayombo.
Vile vile amewataka viongozi wa Vijiji na kata kuwashirikisha Waheshimiwa Madiwani katika michakato ya ujenzi ili waweze kuwahamasisha wananchi kushiriki kujitolea kwani tunaelewa fedha zinazoletwa kwaajili ya ujenzi hazitoshi na ili zitoshe inapaswa wananchi wajitolee kwa nguvu kazi na fedha.
"Acheni majigambo na kujidai nyie wakuu wa idara wasaidieni watu walio chini yenu ili kazi za Serikali ziwezi kufanyika kama inavyoitajika toeni ushauri, maoni na maelekezo ili kazi ziende kwa uharaka" amesema kayombo.
Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg, Selemani Mrope ametoa rai kwa wasimamizi wa miradi inayoendele katika kata au vijiji kuitumia ofisi ya Mkurugenzi kila wanapoitaji msaada.
" msisubiri mpaka mharibikiwe ndiyo mje ofisini watumieni wataalamu wa Halmashauri hatua kwa hatua ili kukamilisha shughuli hizo za ujenzi kwa muda muafaka"amesema Mrope
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa