Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewataka watumishi wa afya kuhakikisha dawa haziishi muda wake kabla ya matumizi.
"Katika matumizi ya dawa zingatieni sana muda wake wa mwisho wa matumizi, kama kuna zile dawa ambazo zinakaribia muda wake kuisha ni lazima zianze kutumika hizo ili ziishe au ni vyema kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili kama kuna uwezekano zisambazwe katika maeneo tofauti tofauti na si kukaa nazo tu mpaka muda wake wa matumizi unaishia wakati huo nyie wataalam wa Kituo au Hospitali husika mnazitazama, kuna wagonjwa wengi sana wanazihitaji hizo dawa ili waweze kupona" Amesema Bi. Zuwena
Ameyasema hayo leo Juni 26, 2024 katika Kikao cha Mrejesho wa Usimamizi Shirikishi Sekta ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya Ruangwa kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya awali na msingi Wonder Kids.
Katika hotuba yake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri Kyaga ameupongeza uongozi na watumishi sekta ya Afya, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuboresha mapungufu yaliyopo katika sekta hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya amemhakikishia Mganga Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi mapungufu hayo ili kuimarisha sekta ya afya walayani Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa