Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ramadhani Kaswa amewataka wanavikundi wa saccos wanaokopa kutoka katika mfuko wa halmashauri kuweza kurejesha mkopo wao kwa wakati, Alisema kuweza kufanya hivyo kwa wakati itasaidia kuwapa nafasi vikundi vingine kuweza kukopa na kubadili kiwango cha maisha kutokana na biashara watakazokuwa wanafanya.
Ameyasema hayo wakati akiongea na kikundi cha vijana saccos mjini Ruangwa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea maendeleo miradi ya Halmashauri, aidha alisema ni vyema wahasibu wa kwenye saccos wapewe mafunzo ya kuweza kuendesha mifumo ya utunzaji fedhana vitabu vya kifedha ili waweze kuandesha saccos zao kitaalamu zaidi na itasaidia kuwa na umakini katika suala za kifedha.
Wakati huo huo Katibu Tawala alitoa pongezi kwa uongozi wa Wilaya kwa ujumla kwa kufanikiwa kujenga shule mpya kwa wakati mfupi na kwa kuzingatia viwango na ubora vya kiufundi‘’Mazingira ya shule ni mazuri kwa mwanafunzi kupatia elimu ila mafundi zidisheni kasi ili shule iweze kumalizika mapema na wanafunzi waanze kutumia majengo yao”alisema
Pia alimtaka Mhandisi wa Maji kufikiria mbinu za kuweza kuwasaidia Shule ya Sekondari Mbekenyera ili waweze kupata jenereta lao la kutumia kupampu maji katika kisima na kuachana na suala la kutumia jenereta waliloazima mara moja.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa