Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amefunga Kikao cha Mkoa cha uchambuzi wa vifo vya wakina mama wajawazito na watoto ( MPDSR) katika Wilaya ya Ruangwa.
Kikao kilianza kufanyika Juni 24, 2024 na kumalizika leo Juni 26, 2024 ambapo kimkoa kimefanyika katika Wilaya ya Ruangwa na kimefanyika katika ukumbi wa shule ya awali na msingi Wonder Kids.
Aidha, Bi. Zuwena amewataka Madaktari wa Mkoa wa Lindi kuunda kundi la madaktari bingwa katika ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kutoa huduma ya afya kwa jamii katika maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Bi. Zuwena amewaomba Wataalam wa afya kufanya kazi kwa moyo mkunjufu ili kuokoa uhai wa wagonjwa mbalimbali hususani wakinamama wajawazito na watoto.
Nae, Mganga mkuu wa Mkoa wa Lindi Dkt. Kheri Kagya ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya Kikao hicho cha MPDSR.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa