Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Mhe. Zuwena Omary amwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack katika hafla ya Mtoko na Mama msimu wa pili na kuwakumbusha wananchi kwamba ukitaka kuwa mama basi jiandae kulea mtoto kimwili na kiakili kwani mpaka kufika hatua ya kuitwa mama si jambo la lelemama.
" Tusichanganye kati ya kuwa mama na kuwa rafiki wa mtoto, ni vyema tukawapatia watoto wetu mahitaji ya msingi na sio ya ziada na kama mama ni jukumu lako kuzungumza na mtoto mara kwa mara ili kujua changamoto anazozipitia"
Ameyasema hayo leo Mei 12, 2024 katika hafla ya Mtoko na mama iliyofanyika katika ukumbi wa Ruangwa Pride Hotel wilayani Ruangwa mkoani Lindi iliyoandaliwa na Binti Lindi Initiative ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mama Duniani ambayo huwa kila Jumapili ya pili ya mwezi Mei kila mwaka
Aidha Mhe. Zuwena ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wanawake na kuboresha huduma za Afya na kutenga 10% ya mapato ya ndani ili kuwapatia mikopo wanawake, vijana na walemavu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu George Mbesigwe ameishukuru Taasisi ya Binti Lindi Initiative kwa kufanya Mtoko na mama katika Wilaya ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa