Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Albert Mwombeki amepokea msaada wa vifaa vya walemavu kutoka katika Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).
Amepokea vifaa hivyo tarehe 15/12/2020 katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Ndg, Mwombeki amesema msaada huo utagawanywa kwa kufuata na taratibu utakaoandaliwa kwa kila kata utapata mgaowake.
Kaimu Mkurugenzi aliishukuru kampuni ya Sigara Tanzania kwa moyo waliyouonesha kuweza kuwasaidia walemavu wa Wilaya ya Ruangwa.
“Zipo wilaya nyingi hapa Tanzania ambazo mngeweza kupeleka misaada hii, ila mmeamua Kuitoa kwa wanaruangwa tunashukuru sana na tunawahakikishia kuigawa kwa walengwa” amesema Mwombeki.
Naye Katibu wa chama cha chama cha walemavu Ruangwa (CHAWATA), ndg, Halfani Lilowa amesema amefurahi kupokea vifaa hivyo kwa hali ya uwazi ambapo wanufaika wameshirikishwa kikamilifu katika zoezi la upokeaji
Aliipongeza Halmashauri kwa kusema imefanikisha jambo hilo kwa utaratibu mzuri wa watu wenye ulemavu wa Ruangwa kuweza kishiriki kushuhudia utolewaji wa vifaa hivyo kwa walemavu na kampuni ya Sigara Tanzania.
Aidha Ndg Liwowa alishukuru viongozi wa kampuni ya Sigara kwa kuona haja ya kuwasaidia watu wenye ulemavu Ruangwa.
Naye Afisa uhusiano wa Kampuni ya Sigara Tanzania ndg, Derick Stanley alieleza wametoa msaada wa baiskeli 28, magongo jozi 50 na fimbo za wasioona 100. Nakwamba wanufaika na msaada huo katika wilaya ya Ruangwa ni watu wenye ulemavu 178 ambao wanatoka katika kata zote zilizopo ndani ya Ruangwa.
Alieleza kwamba Msaada huu umetoka katika mfuko wa Msaada kwa Jamii na nimuendelezo wa kampuni hiyo katika kurudisha faida kwa jamii.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa