Kutokea Wilayani Ruangwa, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imewafikia wananchi wa Kijiji cha Ipingo, Kata ya Luchelegwa, leo Februari 20, 2025, wananchi wamepatiwa elimu kuhusu sheria za ndoa, ardhi, mirathi, haki za mtoto, pamoja na namna ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia ili kuwajengea uelewa wa kutambua na kutetea haki zao.
Kampeni hiyo pia imefanikiwa kutoa ufafanuzi wa masuala ya kisheria yaliyokuwa yanawatatiza wananchi, na wameishukuru Serikali kwa kuwaletea elimu hiyo muhimu, wakisema itawasaidia kulinda haki zao na kukuza ustawi wa jamii yao.
Kampeni hiyo imebeba kauli mbiu isemayo “Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani na Maendeleo”.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa